Mshahara wa Mbunge Wa Tanzania Na Marupurupu
Mshahara wa Mbunge Wa Tanzania Na Marupurupu

Mbunge wa Tanzania hupata mshahara wa msingi na marupurupu mengine kadhaa ambayo yanahusiana na majukumu yake ya kibunge. Kwa kawaida, mshahara huu hujumuisha:
Mshahara wa Mbunge Wa Tanzania Na Marupurupu Yake
Mbunge ni Nani?
Mbunge au wabunge ni wawakilishiwa wananchi katika serikali, hivyo basi tunaweza sema wabunge husimama kana kiunganishi kati ya serikali na raia wanao waongoza, mahitaji na changamoto za wananchi huwasilishwa na wabunge katika serikali yao.
Mbunge Huchaguliwa na Nani?
Mbunge huchaguliwa na wananchi wa jimbo husika baada ya kumpigia kura, Kupitia vyama vyao wabunge hunadi sera na mpipango yao ya kuwatetea na kuwaongoza wananchi mbele ya serikali wakiwa jukwwani na pindi hoja za mmoja kati yao zinapoeleweka na wananchi basi hupigiwa kura na kuchaguliwa kuwawakilisha wananchi hao katika bunge.
Majukumu Ya Mbunge Ni Yapi?
Kama tulivyosema hapo awali mbunge ni mwakilishi wa wananchi katika serikali, kazi za mbunge hufanyika hasa bungeni katikaka kuwakilisha changamoto za wananchi wake na kuhakikisha utekelezaji wa majukumu yote ya serikali kuu kwa wannchi wake.
Mbunge hupokea mshahara kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine wa serikali lakini nje ya mshahara pia mbunge hupokea marupurupu ya ziada kutokana na kazi mbali mbali azitendazo. Hivyo basi makala hii itaenda kuangazia kiwango harisi cha mshahara wa mgunge na marupurupu yake.
Vitu vya Msingi Vya Kuziongatia Kuhusu Mshahara Wa Mbunge
Pindi unapotaka kuuzungumzia mshahara wa Mbunge nilazima uweze kuangazia mambo mbali mbali yanatokana na shuguli zake kama malipo, ukiachilia mbali mshahara wenyewe, Hivyo basi hapa chini tumejaribu kuchanganua malipo yote anayopokea Mbunge kutokana na majukumu yake;
1. Mshahara;
Kama ilivykua kwa wanfakazi wengine katiaka serikali na taasisi za uma mbunge pia hupokea mshahara kama malipo ya msingi kabisa katika kazi zake. Kwa makadilio ya kawaida mbunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania hupokea mshahara unaokadiriwa kua kiasi cha Tsh milioni 3.8 kwa kila mwezi ukiondoa malipo ya ziada.
2. Malipo Ya Ziada
Nje ya malipo ya msingi ya kikazi (mshahara) pia mbunge hupokea pesa ya ziada inayotambulika kama marupurupu amabyo makadilio ya chini ni zaidi ya milioni 7 kwa kila mezi hivyo kuongeza malipo yake ya mshahara hadi kufikia zaidi ya Tsh milioni 11.5 za kitanzania kwa mwezi.
Ukiangalia mchanganuo huo hapo juu utaona jinsi mbunge wa bunge la jamuhuri wa Tanzania anavyopokea mshahara mkubwa sana na kitu hiki ndio kilichopelekea kuibuka kwa mijadala mingi juu ya kuondolewa kwa posho au pesa za ziada nje ya mshahara wa wabunge pindi wanapouzulia vikao vya bunge hii ni kutokana na ukubwa wa posho hizo hivyo kua kama mzigo mkubwa kwa serikali.
Mshahara wa Mbunge na Pesa za Ziada (marupurupu)
Mbunge hupewa msahara kama malipo ya msingi lakini pia hupewa posho kama malipo ya ziada na hiyo huperekea mshahara wake au malipo yake kufikia hadi zaidi ya shilingi milioni 11.5. Posho anazo pewa mbunge ni pamoja na posho za kodi ya nymba, usafiri na posho za viako mbali atakavyo kua nahuzuria
Mchanganuao Wa mshahara wa Mbunge na Posho Zake
- Mshahara – Hupokea kiasi cha shilingi Milioni 3.8 kwa mwezi
- Pesa ya Usafiri- Hupewa shilingi milioni 1 kila mwezi
- Pesa ya Nyumba – Hupewa kiasi cha shilingi milioni 2kwa ajili ya malipo ya nyumba
- Pesa ya Vikao- Kila akiuzulia kikao kimoja hulipwa kiasi cha shilingi laki 2 na elfu 40 – 240,000
Changamoto Kuhusu Mhahara wa Mbunge
Kumekua na mambo kadha wa kadha ambayo yamekua yakiibuka na kujadiliwa kuhusu mishahara na posho za wabunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania na hata kupelekea kusambaa kwa taarifa zisizo sahihi kwa jamii yetu, kama vile kuonngeza kwa mshahara wa wabunge kitu ambacho kilitolewa maelezo na serikali kuu na kukanushwa
Lakini pia wanaharakati na raia wamekua wakijadili hoja hii ya mshahara wa wabunge kwa njia na mawzo tofauti tofauti hivyo kuleta mgawanyiko kati yao kwani wapo wanao amini kua mbunge ana haki na stahiki zote kulipwa kiasi hicho cha pesa ukizingatia majukumu na kazi anazozifanya huku wapo ambao wanakinzana na mshahara huo kwa kudai mshahara wa mbunge umekua mkubwa mno hiyo kipa serikali mzingo mzito kwa kuwazingatia wao na kuacha jamii ikipitia kipindi kigumu kwenye huduma mbali mbali.
Hivyo basi sisi kama Habrika24 tungependa kuishauli jamii kuelewa kwa mapana juu ya mchakato unaopitiwa naserikali kwenye kuunda malipo yote ya mbunge ikiwemo malipo ya msingi (mshahara) na pesa ya ziada ka ma vile posho ya lakini pia serikali inapaswa itumie mfumo wazi ili jamii ielewe juu ya vigezo vya kimsingi vinavyotumika kuweka malipo hayo kwani wanbunge ni zao la wananchi.
Kwa maelezo zaidi unaweza tembelea makala iliyoandikwa kwenye mtandao wa jamii forum kwa kubonyeza HAPA