Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

 0
Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

Njia Rahisi ya Kupunguza Matumizi ya Bando kwenye YouTube

YouTube ni moja ya jukwaa maarufu la kutazama video, lakini matumizi ya data yanaweza kuwa tatizo, hasa ukiwa na kifurushi kidogo cha data. Hapa nitakuonyesha hatua rahisi za kupunguza matumizi ya data unapoangalia video kupitia YouTube App, kwa kutumia simu ya Android au iOS.

Kwa Watumiaji wa Android:

  1. Fungua YouTube App
    Fungua YouTube kwenye simu yako ya Android.

  2. Bofya kwenye Picha yako ya Profaili
    Kwenye kona ya juu ya kulia, bofya picha yako ya profaili.

  3. Enda kwenye Settings
    Kutoka kwenye menyu ya Profile, chagua Settings.

  4. Chagua 'Video Quality Preferences'
    Shuka chini kidogo kwenye settings, na chagua Video Quality Preferences.

  5. Badilisha Settings za Video
    Kwenye sehemu ya "Mobile Network", chagua Data Saver. Hii itapunguza ubora wa video ili kupunguza matumizi ya data.


Kwa Watumiaji wa iOS:

  1. Fungua YouTube App
    Fungua app ya YouTube kwenye iPhone yako.

  2. Bofya kwenye Icon ya Profaili
    Bofya sehemu ya Profile au "You" upande wa chini wa kulia.

  3. Chagua Settings
    Kwenye kona ya juu kulia, bofya Settings.

  4. Chagua 'Video Quality Preferences'
    Tafuta sehemu ya Video Quality Preferences, kisha bofya.

  5. Chagua Data Saver
    Chagua Data Saver ili kupunguza matumizi ya data unapotazama video.


Faida za Kutumia 'Data Saver':

  • Punguza matumizi ya data: Video zitachezwa kwa ubora wa chini, hivyo kupunguza matumizi ya data.
  • Hakuna athari kubwa kwenye video ndogo: Kwa simu ndogo, utaona tofauti kidogo kwenye ubora wa picha.
  • Rahisi kutumia: Huu ni utaratibu rahisi na wa haraka wa kupunguza matumizi ya data bila kuathiri sana uzoefu wa mtumiaji.

Mwisho:

Kama unataka kuona video kwa ubora wa juu, unaweza kuzima Data Saver na kuchagua Auto au Higher Quality, lakini hii itahitaji data zaidi.

TAZAMA MAELEZO YA VIDEO