97 Nafasi za Ajira Serikalini, UTUMISHI - Februari 2025

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI SERIKALINI
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni chombo cha serikali chenye hadhi ya Idara Huru, kilichoanzishwa mahsusi kuratibu mchakato wa ajira kwa watumishi wa umma. Chombo hiki kilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002, iliyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007, kifungu cha 29(1).
DIRA NA DHAMIRA YETU
Dira: Kuwa kituo bora cha Utumishi wa Umma katika kanda.
Dhamira: Kuwezesha ajira ya watumishi wa umma kwa kutumia mbinu za kisasa kwa kuzingatia usawa, uwazi, na sifa stahiki, pamoja na kutoa ushauri kwa waajiri kuhusu masuala ya ajira.
Rasilimali watu ni nguzo muhimu katika utoaji wa huduma za umma, hivyo PSRS inatekeleza jukumu la kuajiri watumishi wa umma kwa haki, uwazi, na kwa wakati, huku ikizingatia ubora na upatikanaji sawa kwa waombaji wote ili kutoa huduma bora kwa Tanzania.
Lengo letu ni kuboresha mchakato wa ajira za serikali kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo na kuimarisha uhusiano mzuri na wadau wetu. Chombo hiki ni mwajiri wa fursa sawa kwa wote.
NAFASI ZA KAZI ZILIZO WAZI
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi mpya za kazi serikalini.
???? BOFYA HAPA KUONA NAFASI ZA KAZI ZA SERIKALI ZILIZOPO MWEZI HUU
???? Ajira Portal Login - BOFYA HAPA
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Waombaji wa nafasi za ajira wanapaswa kuhakikisha kuwa taarifa zao zimesasishwa kwa kutumia Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIN) katika sehemu ya Taarifa Binafsi. Pia, hakikisha taarifa za kitaaluma zimesasishwa kwa kuweka kozi zako kwenye Kitengo Husika.
Ili kuona Hali ya Maombi Yako, tembelea sehemu ya "MY APPLICATION" baada ya kuingia kwenye akaunti yako. Sehemu hii itakuwezesha kuona namba ya usaili kwa waliopata nafasi na sababu kwa wale ambao hawakuitwa.
Kwa maelezo zaidi na kutuma maombi, tafadhali tembelea Ajira Portal.