10 Nafasi kazi za Udereva Serikalini - Februari 2025

NAFASI ZA KAZI: DEREVA DARAJA II (Nafasi 10)
Mwajiri: Halmashauri ya Wilaya Ileje
Muda wa Maombi: 20 Februari 2025 - 6 Machi 2025
Majukumu ya Kazi:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kuhakikisha usalama wake.
- Kuwasafirisha watumishi kwa safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo ya gari inapobidi.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali za ofisi.
- Kutunza rekodi za safari katika daftari la safari.
- Kuhakikisha usafi wa gari unazingatiwa.
- Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na msimamizi wake.
Sifa za Mwombaji:
- Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
- Awe na Leseni ya Daraja E au C na uzoefu wa angalau mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Mshahara: TGS B
Kwa maombi na maelezo zaidi,